Kutengeneza teknolojia huria ya faragha inayolinda uhuru wa kujieleza na kuwezesha mawasiliano salama ya kimataifa.
Tukiwa na bidhaa yetu maarufu, Signal Messenger, tunaamini kuwa kutetea faragha ya mtumiaji kunamaanisha kuweka data mbali na mikono ya mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na mikono yetu, badala ya kudhibiti data yako "kwa uwajibikaji".
Kama mwanachama aliyejitolea wa jumuiya ya programu huria, tunachapisha teknolojia yetu na kushirikisha maarifa ili kuhimiza makampuni mengine kuitumia kwenye bidhaa na huduma zao wenyewe.
Taasisi ya Signal ni shirika lisilo la biashara chini ya kanuni ya 501c3. Tunajivunia uteuzi huo na tuko tayari kuthibitisha kwamba shirika lisilo la faida linaweza kubuni na kuongeza ukubwa kama ambavyo biashara yoyote inayoendeshwa kwa nia ya kupata faida.
Tuliunda Taasisi ya Signal kama kampuni tanzu ya Signal Messenger kwa sababu tunatazamia siku moja kukuza miradi ya kuhifadhi faragha ambayo ina dhamira sawa.
Tunategemea msaada kutoka kwa jumuiya ili kuifanya Signal Messenger iwe programu ya bure kwa mamilioni duniani kote. Je utaiunga mkono dhamira yetu?
Tuliunda Taasisi ya Signal kama kampuni tanzu ya Signal Messenger kwa sababu tunatazamia siku moja kukuza miradi ya kuhifadhi faragha ambayo ina dhamira sawa.
Tunategemea msaada kutoka kwa jumuiya ili kuifanya Signal Messenger iwe programu ya bure kwa mamilioni duniani kote. Je utaiunga mkono dhamira yetu?
Brian Acton ni mjasiriamali na mtaalamu wa programu za kompyuta ambaye alihusika kuasisi programu ya Whataspp mwaka 2009. Baada ya programu kuuzwa kwa Facebook mwaka 2014, Acton aliamua kuondoka kwenye kampuni hiyo kufuatia tofauti zilizohusisha matumizi ya data za wateja na utangazaji uliolengwa ili kuelekeza juhudi zake kwenye mashirika yasiyo ya faida. Mnamo Februari 2018, Acton aliwekeza dola milioni 50 za pesa zake ili kuanzisha Taasisi ya Signal kwa kushirikiana na Moxie Marlinspike. Taasisi ya Signal ni shirika lisilo la faida lililodhamiria kufanya kazi ya msingi kuhakikisha wanawezesha mawasiliano ya kibinafsi, yaliyo salama na yenye kupatikana kila mahali.
Kabla ya kuanzisha WhatsApp na Taasisi ya Signal, Acton alifanya kazi kama mtaalamu wa programu kwa zaidi ya miaka 25 katika kampuni kama Apple, Yahoo, na Adobe.
Moxie Marlinspike ni muasisi wa Signal.
Meredith Whittaker ni Rais wa Signal na mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Signal.
Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 17 kwenye teknolojia, tasnia ya uhifadhi, elimu na serikali. Kabla ya kujiunga Signal kama Rais, alikuwa Profesa wa Utafiti wa Minderoo katika Chuo Kikuu cha New York, na aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kitivo cha Taasisi ya AI Now ambayo alishiriki kuianzisha. Utafiti na kazi zake za kitaaluma zilisaidia kuunda sera ya kimataifa ya AI na kubadilisha mtazamo wa umma kuhusu AI ili kutambua vyema mbinu za ufuatiliaji kwenye biashara na mkusanyiko wa rasilimali za viwandani ambazo AI ya kisasa inahitaji. Kabla ya Chuo Kikuu cha New York, alifanya kazi Google kwa zaidi ya muongo mmoja, ambapo aliongoza timu za bidhaa na uhandisi, alianzisha Kikundi cha Utafiti Huru cha Google, na mshiriki mwanzilishaji wa M-Lab, jukwaa la kupima mtandao linalosambazwa kimataifa ambalo sasa ni chanzo kikubwa zaidi cha data zilizo wazi duniani kuhusu utendaji kazi wa mtandao. Alisaidia katika uratibu Google. Alikuwa mmoja wa waandaaji wakuu waliokuwa wakipambana dhidi ya muitikio hafifu wa kampuni kuhusuiana na AI na madhara yake, na alikuwa mratibu mkuu wa Google Walkout. Ameishauri Ikulu ya Marekani, FCC, Jiji la New York, Bunge la Ulaya, na serikali nyingine nyingi na mashirika ya kiraia kuhusu faragha, usalama, akili unde (AI), sera ya mtandao na vipimo. Na hivi karibuni alimaliza muda kama Mshauri Mkuu wa AI kwa Mwenyekiti katika Tume ya Biashara ya Marekani.